Mabadiliko katika mfumo wa dunia
tangu kuingia kwa karne mpya, ikiwa ni pamoja na utulivu mkubwa wa hali
ya kisiasa barani Afrika na kuongezeka kwa bidhaa muhimu, kama
vikitumiwa vizuri, vitatoa fursa kwa Afrika kuwa nguvu kubwa ya uchumi
duniani. Hayo yamo kwenye utangulizi wa Ripoti ya uchumi kuhusu Afrika
inayoitwa "Kutumia vizuri bidhaa za Afrika: mabadiliko ya viwanda kwa
ukuaji, ajira, na mageuzi ya kiuchumi" ulioandikwa na Carlos Lopes,
naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji
wa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi wa Afrika akishirikiana na
mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma.

Pia wamesema nchi za Afrika zina fursa kubwa ya kutumia vizuri
rasilimali zilizo nazo na bei kubwa ya bidhaa katika soko la kimataifa,
pia zinaweza kutumia fursa zinazotokana na mabadiliko ya uchumi wa dunia
kuinua zaidi uchumi wao kupitia mageuzi ya viwanda na kukabiliana na
umasikini, ukosefu wa usawa, na tatizo la ajira hasa kwa wasomi lukuki waliopo afrika na pia watu wenye elimu ya chini. Endapo fursa hizi
zitatumiwa ipasavyo, zitaisaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa
ushindani, kupunguza kutegemea usafirishaji wa bidhaa ghafi na udhaifu
unaotokana na mambo hayo, hivyo kuibuka kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa
uchumi wa dunia.

Kutokana na ripoti hiyo, Afrika inamiliki karibu asilimia 12 ya
mafuta duniani, asilimia 42 ya madini ya dhahabu, asilimia 80-90 ya
madini aina ya chromium na platinum, na asilimia 60 ya ardhi oevu,
pamoja na rasilimali kubwa ya misitu. Wingi huu wa rasilimali na
kuongezeka kwa mahitaji ya malighafi duniani, serikali katika nchi za
Afrika zinaunda ushirikiano mpya, kukuza uwekezaji kwenye sekta ya
miundo mbinu, na kubadilishana ujuzi na teknolojia. Hivyo serikali za
Afrika zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuendeleza matarajio ya
pamoja kuhusu njia za kutumia vizuri ajenda ya uchumi wa dunia. Kwa
kufanya hivyo, zitakuwa na fursa ya kubadilisha muundo na matokeo ya
utandawazi. Ripoti hiyo imemaliza kwa kusema maendeleo ya viwanda ya
Afrika yanaweza kufikiwa hata katika mazingira ya sasa na uchumi wa
dunia yenye kutokuwa na uhakika.

Kazi iliobaki ni wa afrka wote kuamka usingizini na kuanza kufanya kazi kwa bidii ilikufanikisha malengo ya mtu mmojammoja familia taifa na afrika kwa ujumla... na Nina imani kuwa,, SIKU OTE MAFANIKIO HAYAWI KAMA NDOTO YA USIKU KUOTA UNAGOROFA WAKATI HATA BANDA LA KUKU HUNA...
SHIME VIJANA WENZANGU FURSA ZIPO TUZITUMIE KWA UBUNIFU TULIOPEWA NA MUNGU KUFIKIA MALENGO YETU...
1 comment:
Hi there, this weekend is good for me, as this time i am
reading this enormous informative piece of writing here at my house.
Feel free to visit my web-site ... Ferrars (Http://Upnt.De)
Post a Comment