Tuesday, 31 December 2013

ALOYSIUS PRIMARY AND SECONDARY SCHOOL. SHULE ILIYOLENGA KULETA MAPINDUZI YA ELIMU GEITA NA KANDA YA ZIWA

     Aloysius Primary and Secondary school ni taasisi ya elimu iliyo chini ya kanisa la Roman Catholic Geita. shulee hii ni moja kati ya shule zilizofanya vizuri sana kielim kanda ya ziwa kwa ujumla. katika ziara yake hivi karibuni Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata alipata fursa ya kutembelea taasisi hiyo ya elimu na kuwa mgeni rasmi katika Mahafali maalum ya kuwapongeza wanafunzi wa Darasa la saba walifanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi.
     Kabla ya mahafali hayo Mh. Vicky alipata firsa ya kutembelea shule hiyo na kujionea  hali ilivyo ambapo changamoto zifutazo zinaikabili taasisi ya Aloysius. 1. hakuna Maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea zaidi.2. vyoo ni vichache ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 3. upungufu wa vitabu vya ziada na kiada, 4. hakuna maabara nzuri kwa ajili ya majaribio ya kisayansi 5. hakuna mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaoishi mbali na shule 6. shule haina uzio hivyo kumekuwa na muingiliano baina ya shughuli za kawaida za kijamii na shughuli za kimasomo na hii kupelekea kuwaathiri wanafunzi katika masomo yao.
     katika mahafali hiyo mgeni Rasmi aliahidi kutoa Shilingi Milioni Mbili ili kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili huku akitoa wito kwa jamii na hasa wazazi kusaidia katika kuchangia maendeleo ya kielimu kwa watoto wao na jamii kwa ujumla.

Tazama picha wakati Mh. Vicky Kamata akikagua shule ya msingi na sekondary ya Aloysius.


Mh. Vicky Kamata akikagua madarasa

Ofisi ya Walimu wa shule ya msingi
Vyoo vya wanafunzi ambavyo pia havitoshelezi mahitaji.



     




1 comment:

Anonymous said...

Hello there! This blog post couldn't be written much better!

Going through this post reminds me of my previous roommate!

He always kept talking about this. I am going to forward this information to him.
Fairly certain he'll have a very good read. I appreciate you for sharing!

GEITA DOCUMENTARY

Contributors