Monday, 23 December 2013

WATOTO WANAOLELEWA NA VICTORIA FOUNDATION WALIPOPATA FURSA YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO GEITA. [PAGE 1]

   Na Steven Mruma 

   Watoto wawili wanaolelewa na Victoria foundation Ernest Masuuko Sunguye na Jeremia Julius walipata fursa ya kuwa pamoja na familia zao kwa muda huu wa likizo, watoto hao wanaosomeshwa na kupatiwa matibabu pamoja na huduma zote za msingi na mfuko Victoria Foundation wanasoma shule iitwayo Salvation Army English Medium iliyopo jijini Dar es salam.
   Watoto hao mmoja ambaye ni Ernest anaishi Genge Saba na Jeremia Anaishi Nungwe mkoani Geita.

   Wa kwanza kufika kijijini alikuwa ni Jeremia na hali halisi ilikuwa hiuvi mara tu baada ya kuwasili kijijini.

Jeremia Julius

Jeremia akishuka kwenye Gari alipowasili kijijini kwao, Nungwe mkoani Geita

Akishuka kwenye Gari
Mama yake Jeremia akiwa haamini kumuona tena mwanaye Jeremia

Mama Jeremia akisalimiana na mwanaye
Mama Jeremia akisalimiana na Mh. Vicky Kamata na hapa alikua akimuonyesha jeraha alilolipata mguuni.

Mara tu baada ya kuwasili ndugu jamaa na marafiki walianza kukusanyika nyumbani kwa akina Jeremia

Ndugu jamaa na marafiki wakiwa nyumbani kumsalimia Jeremia
Mh. Vicky akiwa na furaha baada ya kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanakijiji wa Nungwe

Monday, 16 December 2013

Sunday, 15 December 2013

Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape.

Na Steven Mruma kwa msaada wa BBC Swahili.

    Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika mwendazake Nelson Mandela.

      Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.
     Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.
Jeneza lenye mwili wa mzee Nelson Mandela Likiwa limefunikwa na ngozi ikiwa ni ishara ya heshima ya kabila la Thembu

Jeshi likisindikiza msafara wenye mwili wa Mzee Mandela


PICHA ZA SEHEMU ATAKAYOZIKWA MZEE MANDELA LEO.

Na Steven Mruma.

   WAKATI TAARIFA KAMILI YA MAZISHI YA MZEE MANDELA IKIANDALIWA KUPITIA NJIA MBALIMBALI, TUMIA MUDA KUANGALIA PICHA ZA SEHEMU ATAKAYOZIKWA MZEE MANDELA KIJIJINI KWAO QUNU.





Friday, 13 December 2013

TAZAMA PICHA YA HALI HALISI INAYOENDELEA NCHINI AFRIKA KUSINI KWENYE MSIBA WA MZEE NELSON MANDELA.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akitoa heshima za mwisho

Rais Jacob Zuma akiondoka eneo la Union Building jijini pretoria, kwa nyuma ni Graca Machel alivaa nguo nyeusi
Rais wa Zimbabwe Robart Mugabe naye alikuwepo kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela
Rais wa Sli Lanka Mahinda Rajapaska akiondoka baada ya kutoa heshima za mwisho
Aliyewahi kuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki akitoa heshima za mwisho
Mjane wa Mzee Nelson Mandela Graca Machel akiuaga mwili wa aliyekuwa mume wake mzee Nelson Mandela
Aliyewahi kuwa mke wa Nelson Mandela Winnie Mandela akilia kwa huzuni baada ya kuuaga mwili wa Mzee Nelson Mandela
Mwanamitindo mashuhuri Duniani Naomi Campbell akiwa na simanzi baada ya kuuga mwili wa marehemu mzee Nelson Mandela
Winnie Mandela akitoka eneo la kuuaga mwili wa Mzee Mandela , Winnie pia aliwahi kuwa mke wa Mzee Mandela
Maofisa wa jeshi wakijiandaa kubeba jeneza lililobeba mwili wa Mzee Mandela
Maofisa wa Jeshi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mzee Mandela

Monday, 9 December 2013

TAZAMA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA [SASA TANZANIA] UWANJA WA UHURU


Rais Kikwete akiwasili uwanja wa uhuru

Wimbo wa Taifa ukiimbwa

Rais akikagua gwaride

ukaguzi wa gwaride ukiendelea
Rais wa Zanzibar na M/kiti wa baraza la mapinduzi Ali M. Shein akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Gharib Bilal

Rais Kikwete akihutubia wananchi
Vikosi vya usalama vikiwa tayari kwa ukaguzi

Gwaride la kikosi cha akina Wanawake kikitoa heshima zake kwa gwaride la mwendo wa haraka


Kikosi cha FFU wanaume wakipita kwa mwendo wa kasi katika gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ua uhuru wa Tanganyika.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors