Tuesday, 24 September 2013

PICHA: TUKIO LA UGAIDI KENYA [WESTGATE MALL] JESHI LAKARIBIA KUDHIBITI MAGAIDI.. VICKY KAMATA BLOG NA VICTORIA FOUNDATION WATOA POLE.


Polisi wakipambana na Magaidi na Mwili wa mmoja wa raia wasio na hatia waliouwawa ukionekana sehemu ya kuingilia
    Mnamo siku ya Jumamosi Kenya ilikumbwa na Balaa la kuvamiwa na akuuwawa watu zaidi ya 50 kwa kupigwa risasi na magaidi wa kikundi cha al shabab katika Super market maarufu kama WESTGATE MALL Jiji Nairobi.
    Msemaji wa jeshi la Kenya kanali Cyrus Oguna alisema jumapili usiku kwamba jeshi hivi sasa linadhibiti kabisa soko la maduka ya kifahari mjini Nairobi  la Westgate Mall ambako watu 68 waliuwawa na wanamgambo wa kisomali wa kundi la Al-shabab.
mmoja wa majeruhi akpatiwa huduma
Anasema wengi wa mateka waliokuwa wamezuiwa ndani ya soko hilo kubwa wameokolewa lakini inavyoonekana washambuliaji wangali wanawashikiliwa mateka katika sehemu ya maduka na Jeshi la ulinzi la Kenya KDF linadhibiti jengo zima.  Anasema idadi ya watu wanaoshikiliwa mateka haijazidi 10.

Uvamizi wa jengo hilo unaingia katika siku ya tatu jumatatu na jeshi linakadiria kuna kati ya washambuliaji 10 hadi 15.

Wanamgambo wa kundi la Kisomali la Al-Shabab wamedai kuhusika na shambulio hilo na kutishia jumatatu asubuhi kwamba watawauwa mateka wote ikiwa jeshi litaendelea kuwashambulia.

Shambulio hilo lilianza takriban saa sita mchana kwa saa za Kenya  siku ya jumamosi katika soko la maduka ya kifahari la Westgate Mall na kusababisha vifo vya watu 68 na takriban 175 kujeruhiwa kufuatana na maafisa wa serikali.
      Akilihutubia taifa Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa hamasa aliapa  kusimama imara kupambana na kitisho cha ugaidi  akiongeza kusema kwamba vikosi vya usalama vya Kenya vina nafasi nzuri ya kuwashinda waliohusika na shambulio hilo.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata.
 Akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA mchambuzi wa masuala ya kiusalama na kijeshi Godwin Chilewa anasema huwenda kulikuwa na kasoro katika mfumo kamili wa usalama wa Kenya lakini ni vigumu kwa wakati huu kuvilaumu vikosi vya usalama hadi uchunguzi kufanyika.
  Anasema tatizo kuu linaweza kuwa ni ukosefu wa mawasiliano kati ya idara mbali mbali za usalama na namna ya kukusanya habari za kijasusi na jukumu la raia vile vile.

Rais Barack Obama amezungumza na kiongozi mwenzake Uhuru Kenyatta na kutoa rambi rambi zake na kuahidi uungaji mkono wa Marekani katika juhudi za Kenya kupambana na ugaidi.

    "VICKY KAMATA BLOG NA VICTORIA FOUNDATION WANAWAPA POLE WALE WOTE WALIOPOTEZA NDUGU ZAO NA PIA INAWAPA POLE NA KUWAOMBEA WAHANGA WA TUKIO HILO KWA UJUMLA,LAKINI PIA INAWAOMBEA WALIOJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO LA UGAIDI WAPONE HARAKA.

     VICTORIA FOUNDATION NA VICKY KAMATA BLOG KWA UJUMLA INALAANI KITENDO HICHO CHA KINYAMA KWA RAIA WASIO NA HATIA. 

   PIA TUZIDI KUIOMBEA NCHI YETU MUNGU AKAIEPUSHE NA MAJANGA KAMA HAYA AMBAYO YANACHUKUA ROHO ZA WATU WASIO NA HATIA NA KUONDOA NGUVU KAZI YA TAIFA KWA UJUMLA".


PICHA ZA TUKIO HILO, NA JINSI WANAJESHI POLISI KENYA WAKISHIRIKIANA NA MAKOMANDOO WA MAREKANI NA ISRAELI KUWADHIBITI MAGAIDI WALIOPO NDANI


Majeruhi akiwahishwa hospitali
Majeruhi akioka katika jengo akiwa amejeruhiwa vibaya
Maofisa uslama wakipambana na magaidi ndani ya WESTGATE MALL
Mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Magaidi wa kikundi cha Al-shabab
Majeruhi akpatiwa huduma [akipandishwa kwenye ambulance]
mwili wa mmoja wa raia wasio na hatia waliouwawa na magaidi
Magaidi wa kikundi cha al-shabab wakionekana ndani ya jengo hilo wakiendelea kushikilia mateka na kuua watu wasio na hatia


Wahanga wa tukio hilo wakikimbia kunusuru maisha yao na pembeni ukionekana mwili wa mtu aliyeuwawa na magaidi hao
Majeruhi akiwahishwa hospitali
Wanajeshi wakiwa tayari kwa mapambano ndani ya jengo waliopo magaidi wa al-shabab
Hali inatisha ndani ya Jengo la WESTGATE MALL ni machozi na damu
Mwili wa mtu aliyeuwawa ukionekana ndani ya jengo la westgate mall.
Ulinzi usiku na mchana kuhakikisha magaidi hao wanatiwa mbaroni.
Jengo la westgate mall lifuka moshi wakati wa mapambano kati ya maofisa wa usalama na magaidi
Majeruhi akisaidiwa
majeruhi
Mama akiwa na watoto wake waliamua kujificha kwa style hii kuokoa maisha yao
Sehemu ya mgahawa ambao pia ulishambuliwa vikali na magaidi
Rai waliokuwa mateka wakitoka nje ya jengo baada ya kuokolewa na vikosi vya usalama
Wanausalama wakiwa kazini kupambana na magaidi  na mwili wa raia aliyeuwawa na magaidi hao wa al-shabab
Majeruhi akipandishwa kwenye ambulance
Baadhi ya raia waliokuwa wameshikiliwa mateka wakitoka baada ya kuokolewa.



Eneo la maegesho ya magari ikionekana miili ya watu waliouwawa na wengine wakiomba msada kwa ishara ya kujisalimisha.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyata akioa salamu za rambirambi kwa wahanga na pia kuzungumzia tukio hilo kwa ujumla.
Raia wakikimbia kutoka nadni ya jengo baada ya kuokolewa na vikosi vya usalama.
Wanajeshi wakiwa tayari kwa mapambno nje ya jengo
Wanajeshi wa kenya wakizidi kujipenyeza ndani ya jengo hilo kupambana na magaidi hao wa al-shabab.

Thursday, 19 September 2013

PICHA ZA BIRTHDAY PARTY YA VICKY KAMATA.

[Repoted By Steven Mruma]  
  Tarehe 18 septemba ni Birthday ya Mbunge wa viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata, katika siku hiyo ilifanyika paty ya Kumpongeza iliyofanyika nyumbani kwa Shangazi yake Tabata na kisha sherehe hiyo kuhamia Karambezi Sea Cliff Hotel.

   Picha za party iliyofanyika Tabata

zawadi ya keki kutoka kwa Glory
Kata keki tule

Glory akimlisha Mama Keki

Mama akimlisha mwanae Glory Keki



Mambo yalikuwa ni kugonga Chears
Chears, Kutoka Kulia Marry Anicet, na Wadogo Zake Enock Calvin Na Jona

Part ikahamia Karambezi Sea Clif Hotel 

Keki iliyoandaliwa na Sea Clif Hotel
Akifurahia Zawadi kutoka kwa Marafiki zake, Caro Mushi, Rita Mmuya, na Grace Machangu.
Picha Nzuri, akifurahia zawadi kutoka kwa Waheshimiwa Wenzake
"Kata keki tulee"
Caroh Mushi.
Naibu waziri wa Ujenzi Mh. Lwenge

Marafiki zake wapendwa, Naibu waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh. Ummy Mwalimu na Mbunge wa vijana Mh. Neema Hamidi.
Rita Mamuya wa Benki Kuu [wa kwanza kulia] na weheshiwa Wabunge na Manaibu waziri.

Wakiwa katika furaha
Akipokea zawadi kutoka kwa marafiki. kutoka kushoto ni Mh. Dr. Charles Tizeba Naibu waziri Uchukuzi, Mh. Ummy Mwalimu, Mh. Neeama Hamid, Mh. Lazaro Nyarandu Naibu waziri Maliasili na Utalii [haonekani pichani]. na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Lwenge wa kwanza kulia.
Wakifurahia pamoja
 Mbunge Viti Maalum Geita Mh.Vicky Kamata Aliyezaliwa Leo
Mh.Ummy akifuurahi

Dada Yetu Grace Machangu mwenye tabasamu
Dada yetu Caroh Mushi na Tabasamu zito
Naibu waziri Ujenzi Mh. Lwenge
Mh. Dr Tizeba
Mh. Neema Hamid







PICHA NNE ZA BIRTHDAY PART YA NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO Mh. UMMY MWALIMU.

          Hivi karibuni kulifanyika Party ya kumpongeza Naibu waziri wa Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mh, Ummy Mwalimu  katika siku yake ya Kuzaliwa. Party Hiyo iliofana ilifanyika katika ukumbi uliopo Dodoma Hotel.

      VICKY-KAMATA BLOG INAMPONGEZA MH UMMY MWALIMU KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA PIA INAMUOMBEA AWE NA MAISHA MAREFU YENYE BARAKA NA
AMANI.








HALI YA MTOTO ANAELELEWA NA VICTORIA FOUNDATION YAENDELEA VIZURI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI

     Hivi karibuni mtoto Jeremia Julius alifanyiwa upasuaji wa mguu katika hospitali ya CCBRT na hali yake kwa sasa inaendelea vizuri. Upasuaji huo umedhaminiwa na VICTORIA FOUNDATION ambo pia kupitia mfuko wa VICTORIA FOUNDATION ndio inayomlea na kumsomesha Jeremia pamoja na watoto wengine. Akiongea akiwa hospitali hapo mtoto Jeremia alisema anajiskia vizuri na hali yake inaendelea vizuri.. aliyasema hayo alipotembelewa na Mh. Vicky Kamata ambaye ndiye Muanzilishi wa Victoria Foundation.



Mtoto Jeremia Julius

Jeremia Julius [wa pili kutoka kushoto] mmoja kati ya watoto wanaolelewa na Victoria Foundation pamoja na watoto wengine wanaolelewa na Foundation hiyo na Mh Vicky Kamata katika picha ya pamoja.

Wednesday, 18 September 2013

IKIWA LEO NI SIKU YA KUZALIWA VICKY KAMATA: VICTORIA FOUNDATION YAMPONGEZA.


     Ikiwa leo ni Tarehe 18/09/2013 ambayo pia ni siku ya kuzaliwa ya Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata VICTORIA FOUNDATION Imempongeza kwa kutimiza miaka kadhaa siku ya leo.. katika
Foundation hiyo ambayo kazi yake ni kusaidia watoto walemavu, yatima na wenye shida mbalimbali, Kwapamoja wamempongeza kwa kuwalea vizuri na kuwapa msaada mkubwa ambao umefufua matumaini yao ya kupata elimu na maisha bora..
    Pamoja na pongezi hizo kutoka VICTORIA FOUNDATION pia wafanyakazi wa Mh. Vicky kamata ndugu jamaa na marafiki wamemtakia kila la kheri na kumombea Baraka tele na pia Kumuombea kwa MUNGU akampe maisha marefu yenye mafanikio. 
    Katika maadhimisho hayo pia Mh. Vicky Kamata ametoa Zawadi kwa watoto wanaolelewa na VICTORIA FOUNDATION pia kwa wafanya kazi wake pomoja na baadhi ya ndugu na marafiki zake..

 
VICKY-KAMATA BLOG PIA INAMPONGEZA KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA PIA 
 INAMUOMBEA MAISHA MAREFU YENYE BARAKA KUTOKA KWA MUNGU ALIE HAI.



HAWA NI BAADHI YA WATU MASHUHURI WALIOZALIWA SIKU NA TAREHE KAMA YA LEO.

Vicky Kamata

    Ronaldo  
    Ronaldo De Lima
    Jada Smith
    Jada Smith
    Lance Armstrong
    Lance Armstrong
    James Gandolfini
    James Gandolfini
    Xzibit  
    Xzibit
    Frankie Avalon
    Frankie Avalon
    Angela Simmons
    Angela Simmons

GEITA DOCUMENTARY

Contributors