Katibu wa VICTORIA FOUNDATION Ruthvida Daniel (Kulia) akikabidhi kiasi cha Tshs 300,000/= kwa mama mlezi wa kituo cha kulea yatima cha MAUNGA CENTRE kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mama mlezi wa kituo cha MAUNGA CENTRE akionekana ni mwenye furaha baada ya kupokea msaada huo.
Wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha MAUNGA CENTRE.
Monday, 4 March 2013
MH VICKY KAMATA ALIPOTEMBELEA OFISI ZA GAZETI LA HABARI LEO
Mhariri mkuu wa Gazeti la Habari Leo Mr Joseph Kulangwa akisalimiana na Mh Vicky Kamata mara baada ya kuwasili katika ofisi za gazeti hilo.Pembeni ni baadhi ya waandishi wa gazeti hilo.
Mhariri mkuu wa gazeti la Habari Leo Mr Joseph Kulangwa akimuonyesha Mh Vicky Kamata gazeti la Habari leo lililochapishwa siku hiyo.
Mh Vicky Kamata akiwa katika picha ya pamoja na Bi Tuna Abdallah, na Ichikaeli Maro wa Daily News
Wednesday, 27 February 2013
VICTORIA FOUNDATION ILIPOTEMBELEA OFISI ZA SAYED CORPORATION LTD
Kutoka kulia ni Genaral Manager wa Sayed Corporation Mr Mohammed Waheed,Mwenyekiti wa Victoria Foundation hon. Vicky Kamata,Managing Director wa Sayed Corporation Mr Sayed Masood ur Rehman,Katibu wa Victoria Foundation Ruthvida Daniel na Mr
TIB, SIDO kujenga maeneo ya viwanda
BENKI ya Rasilimali Tanzania (TIB) imesaini makubaliano na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo nchini (SIDO) yenye lengo la kushirikiana kuweka miundombinu ya viwanda kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
Mpango huo utawezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda ambao utaanza na mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kutanuka katika miji mingine.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo jijini katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Peter Noni, alisema lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa za viwandani.
“Hapa benki tumebaini kwamba kuna matatizo makubwa kwa mjasiriamali Mtanzania anapojaribu kuwekeza kwa ajili ya uzalishaji.
Vita vya kuondoa umaskini nchini vinategemea uzalishaji. Uzalishaji pia unategemea uwezo wa kupata mikopo kutoka benki.
“Huu utaratibu pia utamwezesha mjasiriamali kukopesheka na taasisi za kibenki, kwa sabau atakuwa na mahala maalumu pa kuzalishia kwa gharama ndogo,” alisema Noni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Michael Laizer, alisema riba ya mikopo inayotolewa na benki nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo kwa sababu ni kubwa mno.
“Riba hizo zinawakwamisha wajasiriamali, zinawarudisha nyuma na pia wanashindwa kupanua biashara zao,” alisema Laizer.
Alisema ushirikiano wa SIDO na TIB utawasaidia wajasiriamali watakaoingia katika mpango huo kupata maeneo ya kuanza uzalishaji kwa gharama nafuu.
Tuesday, 19 February 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)







