Wednesday, 16 October 2013

HAPA NI KATIKA MJI WA KAWASAKI MTAA HUU UNAITWA KAMATA NCHINI JAPAN, AMBAPO WAHESHIMIWA WABUNGE WA KAMATI YA UCHUMI VIWANDA NA BIASHARA WALIPOKARIBISHWA CHAKULA CHA USIKU KWA RAFIKI YAO.

   Kama ulikuwa hujui Chukua hii, nchini Japan kuna mtaa unaitwa KAMATA, ni katika mji wa kawasaki ambapo waheshimiwa wabunge wa kamati ya uchumi wa viwanda na biashara na viongozi kutoka TBS walipata fursa ya kuutembelea walipokaribishwa chakula cha usiku na rafiki yao Mr. Jans. Si hilo tuu bali pia walipata fursa ya kula chakula kwa kutumia vijiko vya DHAHABU.

     Mara baada ya kumaliza kusomewa Taarifa Kutoka Kampuni ya East Afrika Auto Mobile Co,. LTD kutoka kwa Director wa kampuni hiyo Bwana Prosper Japhet waheshimiwa wabunge wa kamati ya Uchumi Viwanda na bishara Pamoja na Viongozi kutoka TBS walikaribishwa nyumbani kwa Bwana Jans ambaye ni rafiki wa karibu wa Bwana Prosper Japhet.
     Bwana Jans Pia ni Director wa Kampuni ya Ukaguzi wa magari [ Pioneer of pre-export inspection] wa Kampuni iitwayo Jans Company LTD. ambayo inafanya kazi ya ukaguzi wa magari yanayoenda zaidi nchini Kenya.

Mh. Vicky Kamata [Kushoto] akipata chakula cha usiku kwa kutumia vijiko vya dhahabu.. kulia ni M/kiti mpya wa bodi ya wakurugenziz TBS.

Mh. Vicky Kamata akiwa mwenye furaha wakati wa chakula cha usiku walichkaribishwa na Bwana Jans.

Wakipata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu Kutoka kulia ni Mr. Jans ambaye ndiye aliyewakaribisha chakula cha usiku anayefuata ni Dada Betty mkaguzi kutoka TBS na Kushoto ni Mr. Luiza ambaye pia ni mkaguzi kutoka TBS.
Mh. Hatibu Haji akipata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu.. kushoto ni Bwana Jans.

Mh. Haribu  Haji akiendelea kupata chakula kwa kutumia vijiko vya dhahabu.

 Huduma ya chakula ikiendelea

PICHA BAADA YA CHAKULA CHA USIKU NYUMBANI KWA MR. JANS

Mh. Vicky Kamata akiwa na Mr. Jans na Mke wa Mr. Jans[Kulia]
Mr. Jans [kushoto] Mh. Hatibu Haji [katikati]i na Mkwe  wa Mr. Jans[kulia]

No comments:

GEITA DOCUMENTARY

Contributors