Sunday, 17 November 2013

PICHA: YALIYOJIRI KARIMJEE WAKATI WA KUAGA MWILI WA DR. SENGONDO MVUNGI JANA

  Na Steven Mruma.

Tazama picha wakati wa kuuaga mwili wa Dr. Sengondo Mvungi viwanja vya karimjee jijini Dar es salam jana ambapo viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, mashirika ya umma na viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Dr. mvungi likiwekwa mahali husika kwa ajili ya kuuaga mwili wake viwanja vya karimjee

Mke wa Dr. Mvungi mwenye nguo nyeupe.
Misa takatifu ya kuaga ikiendelea

Makamu wa Rais G. Bilal akitoa salam za rambirambi

Waziri mkuu M. Pinda akiwa na M/kiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia
Baadhi ya viongozi waliohudhuria
Makamu wa Rais Bilal akiuaga mwili wa marehemu Dr. Mvungi

Waziri mkuu akiuaga mwili wa marehemu

Makamu wa pili wa rais Zanzibar Sharif Hamad akiuaga mwili wa marehemu Dr. mvungi
Rais mstaafu wa awamu ya tatu B. mkapa

Jaji Agustino Ramadhani

Jaji Warioba


Waziri mkuu mstaafu salim A. Salim
Mh. Shamsi V. Nahodha

Jaems Mbatia na mkwe

Steven Wasira

Mh. Mwigulu Nchemba


Prof. Lipumba
Mh. F. Mbowe

Viongozi wengine wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho

Friday, 15 November 2013

HAPPY BIRTHDAY DADA YETU CARO MUSHI.

 Na Steven Mruma.
  Happy birthday Dada Caroh Mushi kwa kutimiza miaka kadhaa MUNGU AKULINDE NA AKUPE MAISHA MAREFU YENYE BARAKA TELE. MUNGU AKUONGEZE HEKIMA NA UPENDO DAIMA Ameen.

PICHA ZA BIRTHDAY PART YA DADA CARO MUSHI.







 




RATIBA YA MAZISHI YA DR. SENGONDO MVUNGI.


LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE



Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN


KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE


Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji

Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili wa Marehemu

Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee

Saa 5:45 – 6:55 mchana
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani


Saa 6:55 – 8:40 Mchana
Kuaga Mwili wa Marehemu


Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi


KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI


Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu

Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro.
Na huko ndipo yatakapofanyika mazishi ya Dr. Mvungi.

Thursday, 14 November 2013

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI NYUMBANI KWA MAREHEMU DR. SENGONDO MVUNGI HUKO KIBAMBA.

Rais Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Dr. Mvungi

Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma wakimfariji mke wa Dr. Mvungu Anna Mvungi mwenye nguo nyeupe nyumbani kwa marehemu Kibamba.
Rais Kikwete  wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na M/kiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba kushoto, wa pili kulia ni M/kiti wa NCCR - Mageuzi James Mbatia na kulia ni Mjumbe tume ya mabadiliko ya katiba na waziri mkuu mstaafu Salm Ahmed Salum

Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilali akimpa pole mke wa Dr. Mvungu Anna Mvungi alipotembelea kuwafariji nyumbani kwa marehemu Kibamba.
Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal akisaini kitabu cha Mombolezo
M/kiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kibamba
Baadhi ya wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba wakitoa pole kwa mke wa marehemu

Baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu Dr. Mvungi

Tuesday, 12 November 2013

TANZIA: DR. SENGONDO MVUNGI AFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MATIBABU AFRIKA KUSINI


 Hayati Dr. Sengondo Mvungi enzi za uhai wake

Dr. Mvungi akiwa hospitali baada ya kujeruhiwa na majambazi kabla ya kufariki mchana wa leo.
Habari kutoka afrika kusini alikopelekwa dr. Sengondo  Mvungi baada ya kujeruhiwa na majambazi walipovamia nyumbani kwake hivi karibuni kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hasa maeneo ya kichwani.
   Hali Dr. Mvungi alibadilika na kuwa mahututi na kupelekea kupoteza maisha, tayari viongozi mbalimbali wa tume ya katiba akiwemo M/kiti wa tume hiyo Jaji J. Warioba wameshafika nyumbani kwa marehemu.

                 BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Sunday, 27 October 2013

MAHAFALI YA KIHISTORIA SHULE YA WAMA NAKAYAMA,WAHITIMU NA VICKY KAMATA WAKONGA NYOYO ZA WATU, MGENI RASMI RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ASHUKA JUKWAANI KUCHEZA.

   Imeandikwa na Steven Mruma.  

Siku ya jumamosi ilikuwa ni mahafali ya kwanza na ya kihistoria ya shule ya sekondari ya wama nakayama iliyopo Rufiji, shule hii ni moja kati ya foundation ya Mama Salma Kikwete [WAMA] ambayo inasomesha wanafunzi zaidi ya 800, katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa Mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya M. Kikwete.
    Katika mahafali hayo yaliambatana na burudani mbalimbali za muziki pamoja na vikundi vya sarakasi nk. moja kati ya wasanii waliotoa burudani ya aina yake ni Msanii na pia Mbunge wa Viti Maalum Geita Mh.Vicky Kamata ambaye wimbo wake ulikonga nyoyo za wageni waalikwa pamoja na Mgeni rasmi ambaye aliamua kushuka kutoka jukwaa kuu na kuanza kucheza pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Msanii mwingine aliyetoa burudani ni Mjomba Mrisho Mpoto.
   Katika mahafali hayo pia yalihudhuliwa na Mwenyekiti mtendaji wa mashirika ya IPP Bwana Reginald Mengi ambaye alitoa ahadi ya kuchangia shilingi Bilioni moja [1] ndani ya miaka mitano [5] akiwa na maana ya kutoa milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano.
Msanii na pia Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata akiimba pamoja na wanafunzi wanaoagwa [kidato cha kwanza hadi cha tatu]

Msanii na pia Mbunge Vicky Kamata akiendelea kutoa burudani

Wanafunzi wanao waaga wenzao wa kidato cha nne wakiwa tayari kuimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wakiongozwa na Msanii na pia Mbunge Vicky Kamata
M/kiti mtendaji wa makampuni ya IPP Media Bwana Reginald Mengi akiwa na Bwana Hasheem Ghalib ambao pia ni wafadhili wa  WAMA NAKAYAMA
Mh. Mbunge wa Viti maalum na Msanii wa Muziki Vicky Kamata akiimba wimbo maalum na wahitimu 

Wahitimu wakiimba kwa huzuni wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao pamoja na Mh Vicky Kamata, wimbo huu ndio pia uliokonga nyoyo za wengi na hata mgeni rasmi aliamua kushuka kutoka jukwaa kuu na kujumuika kucheza  
Mgeni rasmi na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwa ameshuka kutoka jukwaa kuu kucheza pamoja na wahitimu na wageni waalikwa.

Rais Dk. Jakaya M. Kikwete akiwa mwenye furaha wakati aliposhuka kutoka jukwaa kuu kujumuika katika muziki uliokua ukiimbwa na Msanii na pia Mbunge wa Viti maalum Geita Mh. Vicky Kamata [kulia ni Mama Salma na Mh. Vicky Kamata aliyeshika Mic]

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Salma Kikwete pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors