 |
| Baadhi ya wakuu wa SADC |
RAIS wa Malawi, Joyce Banda
amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha demokrasia, amani na usalama
katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC).
Banda alitoa pongezi hizo wakati
akihutubia Mkutano wa 33 wa Wakuu wa SADC baada ya kukabidhiwa nafasi ya
uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Msumbiji, Dk Armando Guebuza.
“Wananchi wa Malawi, mimi na SADC
tunampongeza Kikwete kwa kuimarisha amani, demokrasia na usalama katika jumuiya
katika kipindi chake cha uongozi (wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na usalama “Pia Rais
wa Msumbiji, Armando Guebuza katika uongozi wake wa uenyekiti alishirikiana na
Kikwete kushughulikia matatizo ya kisiasa na kuufanya ukanda wa nchi za SADC
kuwa na amani,” alisema Rais Banda, ambaye nchi yake ina mgogoro na Tanzania upand
wa ziwa Nyasa.
 |
| Rais Kikwete na Rais Joyce Banda wa Malawi |
Mgogoro
huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi bila kushauriana na Tanzania, kutoa
leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la Ziwa upande
wa Tanzania na kuibua mgogoro huo.
Chanzo cha mgogoro huo unaoshughulikiwa na jopo
la marais wastaafu wa Afrika; Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Joachim Chisano (Msumbiji),
Festus Mogae (Botswana) na wanasheria saba wa kimataifa, ni mikataba yenye
utata iliyoachwa na wakoloni. Alisema ambao ndo waloigawa mipaka hiyo wakati wa
ukoloni.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha
uongozi wa Rais Kikwete katika asasi hiyo ya siasa, ulinzi na usalama aliweza
kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe, ambao Robert Mugabe
ameshinda kuingoza nchi hiyo kwa muhula mwingine na kumbwaga mpinzani wake
mkubwa na aliyekuwa waziri mkuu Morgan Tvshangirai.
Amefanikisha pia kuanza
kwa mchakato wa amani na kuatikana kwa muafaka wa kisiasa nchini Madagascar.
Pia katika kipindi chake, alifanikisha kupelekwa kwa
wanajeshi wa kulinda amani katika mji wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) ambapo waasi wa M23 wanapambana na wanajeshi wa serikali. Wanajeshi hao
wa kulinda amani wametoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Rais Kikwete amekabidhi madaraka hayo jana kwa
Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba. Rais huyo wa Malawi Bi. Joce Banda ameahidi amani, Akizungumzia mkakati
wake wakati wa uongozi wake wa mwaka mmoja kama Mwenyekiti wa SADC, Banda
alisema ili ukanda wa SADC uwe na amani na usalama ni lazima nchi wanachama
zipambane na umasikini.
“Lazima tuimarishe siasa za ndani za
nchi zetu, tuwe wavumilivu wa kisiasa na tusaidie wanawake wasiwe nyuma,”
alisema. Aliahidi kuimarisha jumuiya za kikanda pamoja na kilimo kwa maelezo
kuwa kilimo ndicho mwajiri mkuu wa wananchi wa nchi za SADC.
“Nitahamasisha
kilimo kiboreshwe ili wananchi wa SADC waweze kuendesha kilimo cha biashara na
pia sekta binafsi waingie kwenye kilimo na tupate masoko mapya ya bidhaa za
kilimo nje ya mipaka ya ukanda wetu”.
Alitaka katika ukanda wa jumuiya ya SADC
kuboreshwe mwingiliano wa wananchi wa nchi za ukanda huo. Alisema haiwezekani
kuboreshwa kwa jumuiya za kikanda bila kuruhusu mwingiliano huru wa wananchi
wake.
Rais Banda alitaka wanawake wapewe nafasi katika
uongozi na kujengewa uwezo katika kuimarisha uchumi na kuondokana na umasikini
na kusisitiza kuwa, “wanawake ndiyo wanaopambana na umasikini, wanabakwa,
wanakabiliwa na unyanyasaji na wengi wamepoteza utu wao”.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja
wa Afrika (AU), Dk Nkosazana Dlamini- Zuma alizitaka nchi za Afrika kuimarisha
miundombinu ili mazao ya wakulima yaweze kusafirishwa pamoja na kuboreshwa
kilimo, uwekezaji na kujengwa kwa viwanda.“Lazima tufanye kazi pamoja kuwahakikishia
chakula watu wetu wa SADC na Afrika haiwezi kuendelea bila kuweka wanawake kila
maeneo na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili za tatizo la ajira kwa
vijana, umasikini, sekta duni ya viwanda na tatizo la kutokuwepo usawa wa
kijinsia,” alisema Zuma.