Friday, 2 November 2012

MAFUTA BADO UTATA



WAKATI Kampuni ya uratibu ya uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PIC) ikipigiana chenga na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kuhusu uhaba wa mafuta nchini, serikali imeagiza kusitisha kusafirisha mafuta nje ya nchi.
Agizo hilo la serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Maswi, alipokutana na Bodi ya PIC pamoja na Ewura mbele ya waandishi wa habari na kuwataka waeleze sababu za kuadimika kwa nishati hiyo nchini.

TOA MAONI YAKO YA KATIBA MPYA KWA SMS SASA..



TUME ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ‘sms’ kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao ni 0715-081508, 0767-081508, 0787-081508 na 0774-081508.

Monday, 29 October 2012

VINARA WA ROCK CITY MARATHON



MWANARIADHA anayekuja juu kwa kasi, Mwita Kopiro, wa Mwanza na Mary Naali wa Arusha, jana waliibuka washindi katika mbio za Nusu Marathon za Rock City zilizofanyika jijini Mwanza jana.

Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume, akitumia saa 1:04:02, huku Mary anayetoka klabu Skytel akishinda kwa wanawake akitumia saa 1:16:33.

Waliofuatia kwa wanawake ni Sarah Ramadhan Arusha (1:16:37), Anastasia Msindai Arusha (1:19:05), Failuna Mohamed Arusha (1:19:20), Musengimana kutoka Rwanda (1:22:09), Banuelia Brighton Holili Kilimanjaro (1:22:15), Dorcas Jepchirchir Kenya (1:26:12), Sarah Kavina JKT Arusha (1:36:37), Furaha Sambeki Tanzania (1:36:55), na Grece Jackson (1:40:53).

Thursday, 25 October 2012

NSSF YAZITAKA Manchester United, Chelsea,Real Madrid



SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeanzisha mchakato wa kujenga kituo cha kuibua vipaji vya soka nchini kwa kutumia jina la klabu mojawapo kubwa ya barani Ulaya.

Mkurungenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, aliiambia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), jana kwamba, kwa sasa wapo katika mazungumzo na timu kubwa za Real Madrid ya Hispania, Manchester United, Liverpool na Chelsea za England.

Wednesday, 24 October 2012

NDEGE YA JESHI YAANGUKA, MMOJA APOTEZA MAISHA


MWANAJESHI mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya ndege ya mafunzo waliyokuwa wamepanda maofisa wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) kupoteza mwelekeo na kuanguka katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe, alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa haijaruka, lakini maelezo yake yameonekana kujichanganya.

Alisema wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka ikiwa na maofisa wa mafunzo wawili, ilipoteza mwelekeo na kuserereka na kuelekea ndani kwenye hanga kitendo kilichowafanya waamue kujinusuru maisha yao.

“Ndani ya hanga hilo kulikuwa na ndege nyingine mbili, lakini hata hivyo tunashukuru hakuna madhara yaliyotokea, kila kitu kiko salama,” alisema Kanali Mgawe.

Alisema wanajeshi hao, kila mmoja aliamua kuchumpa kwa mwamvuli ambapo Kapteni Magushi alianguka juu ya paa la jengo lililokuwa karibu na eneo hilo ndipo alipopoteza maisha.

Alimtaja mwanajeshi aliyenusurika katika tukio hilo, kuwa ni Kapteni Kwidika, ambaye amekimbizwa katika hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wanajeshi hao walikuwa katika shughuli zao za mafunzo ya kawaida.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors