Saturday, 31 July 2010

Duh, kumbe kuku na yai wakwanza kutokea ni kuku!!!


Wanasayansi wa Ulaya wametatua ule uzushi wa kipi cha kwanza kutokea kati ya kuku na yai.
"Imekuwa ikizoeleka kufikirika kuwa yai lilikuja kabla ya kuku"
Watafiti kutoka Scotland na Uingereza walitumia Supercomputer iitwayo HECToR kwa kulchunguza gamba la yai la kuku na kugundua uwepo wa protein ambazo hutumika katika utengenezaji wa awali kabisa wa yai tumboni mwa kuku.Na protein hiyo hupatikana kwa kuku tu.
Kwa hiyo kuku alikuja wa kwanza na yai lilifuata.

Monday, 28 June 2010

Albam 10 na Miaka 10 ya African Stars 'Twanga Pepeta'


Mwanamuziki mwalikwa katika bonanza la mafanikio ya albamu 10 na kutimiza miaka 10, tangu kuanzishwa kwa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Ramadhani Masanja 'Banza Stone' (kushoto) akienda sambamba kiongozi wa bendi hiyo, Lwiza Mbutu wakati wa bonanza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club, jana.

Thursday, 24 June 2010

MAONYESHO YA ELIMU NA TAALUMA NDANI YA DIAMOND JUBILEE


Maonyesho ya ELIMU NA TAALUMA TANZANIA yameanza leo katika ukumbi wa Diamons Jubilee-DSM.


Wawakilishi wa Tanzania House Of Talent wakiwa katika picha ya pamoja katika Maonyesho ya Elimu na Taaluma Tanzania.Watembelee kupata elimu zaidi kuhusu Sanaa na Muziki wetu.

Pia tembelea banda la TANZANIA SCHOOLS COLLECTION waweze kukusaidia katika suala zima la kupata elimu bora,kwa kukupa taarifa kuhusu shule mbalimbali nchini kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu.


JE wewe ni mhitimu na unatafuta ajira??Basi tembelea banda la PROACTIVE EMPLOYMENT SOLUTIONS katika maonyesho ya Elimu na Taaluma Tanzania wakusaidie..

Wanafunzi wa LadyBird Pre-School wakionyesha taaluma yao ya kuchora katika Maonyesho ya Elimu na Taaluma yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dsm.

Monday, 14 June 2010

Changia Damu,Okoa Maisha..


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Biafra wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya wahamasishaji katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani.


Mmoja wa wachingiaji damu akiwa amekaa tayari kwa ajili ya kuchangia damu katika maadhimisho ya Wachangia Damu Duniani ambayo hufanyika kila tarehe 14/06.Kitaifa Kanda ya Mashariki yalifanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni-DSM.

Friday, 11 June 2010

Afrika Kusini yalazimisha sare na Mexico


Siphiwe Tshabalala akitandika mkwaju kuipatia Afrika Kusini goli la kwanza.

Wenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini, wameanza michuano hiyo kwa matumaini baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mexico.

Mexico wenye uzoefu mkubwa wa kucheza katika Kombe la Dunia walianza kwa kumiliki mpira kwa kipindi kirefu, lakini walishindwa kumalizia nafasi zilizopatikana.

Baada ya mapumziko, kocha wa Afrika Kusini, Carlos Alberto Parreira, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Lucas Thwala na kumwingiza Tsepo Masilela.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors