Monday, 22 June 2015

UWT MKOA WA GEITA WANUFAIKA NA BAISKELI ZAIDI YA 500 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLIONI 78 KUTOKA KWA MBUNGE WA VITI MAALUM GEITA MH.VICKY KAMATA.

     Mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita Mh. Vicky Kamata ametoa baiskeli kwa viongozi wa kata zote za Mkoa wa Geita, Baiskeli zinazokadiriwa kufikia 500 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Millioni 78 za Kitanzania..
     Akikabidhi baiskeli hizo katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Abdullahaman Kinana alisema ni wakati sasa akina mama na viongozi wa UWT waliopata baiskeli hizo wazitumie katika shughuli mbalimbali za kuwafikia wananchi na kuwasaidia kutatua matatizo yao pamoja na kazi ya kujenga chama.
    Nae Vicky Kamata alipokua akizungumza alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta kumwagia sifa kemkem katibu mkuu huyo wa CCM kwa kujitoa kwa dhati kabisa kukipigania chama,, "Natoa Baiskeli hizi kwa viongozi wote wa UWT mkoa wa Geita kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na katibu mkuu, ninatoa pongezi za dhati kabisa kwani kulingana na nafasi yake angeweza kwenda nchi mbalimbali kula bata lakini aliacha yote ameacha familia yake anazunguka Tanzania nzima jua lake, joto lake, mvua yake, baridi yake lakini hajali" alisisitiza Mh Vicky alipokua akiongea kwenye  mkutano wa Hadhara uliofanyika viwanja vya Nyankumbu Geita.













Sunday, 10 May 2015

PICHA ZA MAHAFALI YA JULIANA MMOJA WA WAIMBAJI WA KUNDI LA J.SISTERS ALIPOHITIMU SHAHADA YA KWANZA YA PHAMARCY HUKO NCHINI MAREKANI.

Steven Mruma,,

      Mmoja kati ya waimbaji wa kundi la muziki wa injili la J.Sisters, Juliana Julius Mshama amehitimu mafunzo ya shahada ya kwanza ya Pharmacy katika chuo cha Liberty universirty of lynchburg va. Amerika huko nchini marekani. Pamoja na Juliana chuoni hapo pia wamesoma ndugu zake wawili Jennifer na Jackline huku mdogo wao Jesca akitarajia kujiungana na chuo hicho hivi karibuni.
      Juliana na ndugu zake wamekua miongoni mwa wasanii wa muziki wa injili wachache wasomi zaidi wakiwakilisha vema kundi lao la muziki J.Sisters waliotamba na nyimbo nyingi ikiwemo shuka bwana.

ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA KATIKA MAHAFALI ILIYOFANYIKA HUKO NCHINI MAREKANI
Juliana J. Mshama mmoja wa waimbaji mahiri wa kundi la J.Sisters

Juliana (aliyevaa joho) akiwa na ndugu zake Jennifer na Jackline pamoja na  jamaa na marafiki zake wakati wamahafali yake pamoja na Baba yao Julius Mshama (mwenye kofia nyeusi)







Monday, 4 May 2015

PICHA ZA MH SAMWELI SITTA KATIKA IBADA YA KUMSHUKURU MUNGU KWA MIAKA YAKE 30 YA UTUMISHI JIMBONI URAMBO MASHARIKI NA MIAKA 47 YA NDOA YAKE.

Na Steven Mruma..

     Usipomshukuru Mungu utamshukuru nani mwingine?
Mh. Samweli na Mkewe Magreth Sitta jana walifanya sherehe fupi ya kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 47 ya ndoa yao na miaka 30 ya utumishi wao katika jimbo la Urambo mashariki.
    Shukrani zingine ilikua ni pamoja na kutumikia serikali kama spika wa Bunge na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ambapo alifanikisha kupatikana kwa katiba inayopendekezwa..
    katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na baadhi ya viongozi na wabunge ikiwemo Mh. Vicky Kamata aliyeimba wimbo maalum aliotunga kwa ajili ya Mh. Samweli Sitta na familia yake, ambao ndio ulikua wimbo maalum wa shukrani.. wengine waliohudhuria ni Mbunge David Kafulila na Mh. L.Lusinde, ndugu jamaa na marafiki.

YAFUATAYO NI BAADHI YA MATUKIO KATIKA PICHA YA HAFLA HIYO FUPI YA SHUKRANI.


















Monday, 27 April 2015

PICHA ZA USIKU WA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IKULU.

Picha na Steven Mruma. 


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa Ikulu



Mh. Vicky Kamata akisalimiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Mh. Philip Mangula

Mh. Vicky akiteta jambo na Mh. Mangula












Steven Mruma

Wednesday, 15 April 2015

KWAPAMOJA TUSAIDIANE KUPAMBANA NA AJALI ZINAZOMALIZA WATANZANIA WENGI:



Kila kitu kinawezekana,, Hivi ndivyo Shule ya Jangwani ilivyoshinda tuzo ya ujasiriamali..

MAKALA YA MWANANCHI.

Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Jangwani wakionyesha baadhi ya kazi wanazojifunza. Picha na Maimuna Kubegeya

Programu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi, ni malumu kwa ajili ya kuwaandaa kuingia kwenye dunia ya biashara

        Hivi karibuni, Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, iliibuka mshindi kwenye shindano la ujasiriamali kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo lilitokana na mafunzo ya miezi mitatu kuhusu ujasiriamali yaliyokuwa yakitolewa kwa wanafunzi wa shule zaidi ya 10 za jijini humo na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Junior Achievment Tanzania (JAT).
Kufikia kilele cha mafunzo hayo, shule zilizoshiriki zilipata wasaa wa kushindana na hatimaye, Jangwani iliibuka kinara na kujishindia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Gabon Disemba mwaka huu.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Shule ya Benjamin Mkapa, huku Chuo cha Ufundi Stadi Kipawa kikichukua nafasi ya tatu.
Shule nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Shule za sekondari za Pugu , Kibasila, Middland, Tegeta na Jitegemee pamoja na vyuo vya Paradgims, Chuo cha Ufundi Stadi Kipawa na Chang’ombe.
Mkurugenzi wa kampuni E-Smart Creators ya Jangwani, Sonia Apolo, anasema kuwa siri pekee ya ushindi wao ni ule ubunifu waliotumia katika kutengeneza bidhaa yao ya kipekee.
“Mkaa wa makaratasi ndio bidhaa iliyotupa ushindi na hata kuweza kupata nafasi hii. Tulitumia muda wetu mwingi kujifunza tukiwa kwenye programu hii ya mafunzo na baada ya kufuzu, tuliuingiza kwenye biashara” anasema na kuongeza:
“Mkaa huu unatumika kwa kupikia na hata kuongeza joto majumbani kwa maeneo yenye baridi, hivyo mipango yetu ya baadaye ni kuhakikisha bidhaa yetu inawafikia Watanzania wengi.”
Pamoja na bidhaa hii ya kipekee, shule ya Jangwani ilionyesha bidhaa zake nyingine walizoziingiza sokoni ikiwa ni baada ya kuuza hisa na kupata mtaji wa kuendesha biashara yao.
Miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni pamoja na fulana zilizochapishwa nembo ya kampuni yao, bangili, hereni na vifaa vya shule.
Shindano la ujasiriamali
Mratibu wa programu hiyo, Hamis Kasongo anasema kuwa shindano hilo ni miongoni mwa programu za kawaida zinazoendeshwa na taasisi yake, zikilenga kumtayarisha kijana wa Kitanzania kuingia kwenye ulimwengu wa biashara, huku akijua thamani halisi ya pesa na matumizi yake.

“Tumekuwa tukiendesha programu mbalimbali kwa vijana wa rika tofauti tofauti. Baadhi yake ni pamoja na program ya kampuni, ‘Its tyme’, Job shadow na nyingine nyingi zikiwa na nia ya kumuandaa kijana kupambana na ulimwengu wa kibiashara” anafafanua.
Anasema kuwa wanafunzi hufundishwa jinsi ya kuendesha kampuni, wakianza kujitengenezea mfumo wa kampuni na baadaye kununua hisa zinazowawezesha kuanzisha mradi utakaweza kuwaingizia pesa.
Katika mfumo huo, anasema kunakuwa na wakurugenzi na pia mameneja wanaoratibu kazi za kila siku na hatimaye kufanikiwa kutengeneza faida.
Program hiyo inayoendeshwa kwa miezi mitatu pia hutoa fursa kwa vijana hao kujifunza jinsi ya kuandika michanganuo ya kibishara na pia ripoti wakati wa kufunga hesabu za kampuni.
Meneja wa masoko wa benki ya Baclays, ambao ndio wadhamini wa program hiyo, Joel Bendera, anasema kuwa mpango wao ni kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata mafunzo hayo, kwani licha ya kuwapanua kiuelewa, yatasaidia kuwapa ujasiri wa kujiajiri mara wamalizapo masomo yao.
“Tangu kuanzishwa kwa programu hii mwaka 1998, tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wengi zaidi wanafikiwa. Tutahakikisha kila mwaka tunakuwa bega kwa bega na JAT, ili kufikia malengo yetu” anaeleza,
Ushuhuda
Issac Uswege ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,tawi la Mbeya ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliopitia programu hiyo.
“Nilifanya programu hii nikiwa Shule ya Sekondari Tambaza wakati ule nilitekeleza majukumu kama mkurugenzi. Nikiwa katika wadhifa wangu huo nilifanikiwa kutengeneza mikakati iliyoboresha kampuni yetu na hata kufanikiwa kupata ushindi kwenye mashindano kama haya” anafafanua
Anasema mafunzo hayo yalimjenga kiujasiriamali hata kumshawishi kufungua biashara yake binafsi mara baada ya kumaliza kidato cha sita.
“Nilianza na biashara ya pikipiki na baadaye niliziuza na kununua bajaji. Nilianza kufanya biashara wakati nasubiri matokeo yangu lakini hata baada ya kutoka matokeo na kufaulu, bado niliendelea na biashara huku nikisoma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe” anasema na kuongeza.
“Hivi sasa nimemaliza masomo nimeajiriwa kama mwalimu wa biashara, lakini pia naendelea na ujasiriamali. Kwa sasa nimejikita katika kilimo cha miti” anafafanua. Junior Achievment ni taasisi iliyoanzishwa nchini Marekani na imeenea katika nchi 121 duniani, zikiwamo 15 zilizopo barani Afrika. Hadi sasa imetoa mafunzo kwa vijana zaidi ya vijana 25,000.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors