Wednesday, 9 July 2014

BAADA YA KUTAMBULISHA KILICHOTOKEA KATIKA SIKU YA KUZALIWA YA MTOTO WA MH. VICKY KAMATA MZIGO MZIMA HUU HAPA. ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MUHIMU YALIYOTOKEA KATIKA HAFLA HIYO FUPI YA KUMPONGEZA GLORY.


Picha Habari na Steven Mruma

MAANDALIZI YA KUPANGA VITI NA MEZA PAMOJA NA MAMBO MUHIMU YALIENDELEA JAPOKUWA HALI YA HEWA ILIONEKANA KUTOKUA SHWARI SANA

VITI VYA WATOTO NA VIFAA MBALIMBALI VILIENDELEA KUFUNGWA NA WATAALAM WAKISASA

MAANDALIZI YALIZIDI KUPAMBA MOTO KILA MUDA ULIPOSONGA

MAANDALIZI YAKIENDELEA KWA USTADI MKUBWA

MAANDALIZI YAKIENDELEA
MTARIBU WA SHUGHULI NZIMA AKIWA KATIKA PILIKAPILIKA ZA KUWEKA MAMBO SAWA HASA YA MALIPO NK
WATOTO WAKIENDELEA KUFANYA YAO
WATOTO WALIENDELEA KUJIPANGA HUKU WAKIPEWA MAELEKEZO NA MH VICKY
 DJ AKIWEKA MAMBO SAWA





FUNDI JAMES ALIHUSIKA KATIKA UTAALAM WA MAMBO YA UMEME NA TAA ZA KISASA

 
WATOTO KWA WAKATI WOTE HUO WALIKUA WAKIFANYA YAO
JIONI ILIPO INGIA SHUGHULI ILIANZA RASMI

SHEREHE ILIANZA KWA DUA NA WIMBO WA BIRTHDAY ULIIMBWA MISHUMAA IKAZIMWA NK..

MISHUMAA IKIZIMWA NA MTOTO GLORY

MAMA GLORY AKIMSAIDIA GLORY KUKATA KEKI

GLORY AKIKATA KEKI
WATU WALIANZA KUJICHANA KWA KEKI..
GLORY ALIENDELEA KUWALISHA KEKI WAGENI WAALIKWA NA KILA MTU ALIPATA KEKI NA SI RAHISI KUWEKA PICHA ZOTE KWANI WAGENI WALIKUWA NI WENGI SANA NA KUONA PICHA NYINGINE ANGALIA HABARI ILIYOPITA


PACHA WA MH. VICKY KAMATA DADA YETU ANJELA MSANGI ALIKUA MC WA SHUGHULI HIYO NA ALITISHA SANA
WATOTO PAMOJA NA MTOTO GLORY WALIANGUSHA SHOO YA KUFA MTU NI NOUMAA SANA

WATU WAZIMA WALIUNGANA NA WATOTO KUCHEZA MUZIKI
BAADA YA SHOO YA WATOTO PALIPIGWA SHOO ZINGINE MBILI KALI SANA JE UNAJUA NI SHOW YANANI NA NANI?  VIJANA WA MBONA UNACHELEWA CHELEWA NA MH. VICKY WALISABABISH VYA KUTOSHA.
VIJANA WA MBONA UNACHELEWA CHELEWA WAKIPIGA SHOO KALI SANA
HII ILIKUA NI KWA MARA YA KWANZA MH. VICKY KAMATA KUFANYA SHOO YA WIMBO WAKE MPYA WA MOYO WA MTU KICHAKA
SHOO KALI IKIENDELEA NA MWISHON MH ALIONGEA NENO MOJA TU, HUA HAFANYI SHOO HOVYO NA IKITOKEA AKAFANYA SHOO BASI NI SEHEMU ADIMU TU NA KATIKA MATUKIO ADIMU TU.
SHOO KALI YA MH. VICKY KAMATA IKIENDELEA


HUYU NI MTOTO ANAYELELEWA NA VICTORIA FOUNDATION JAPO KUWA NI MLEMAVU LAKINI NI MPIGA PICHA MAKINI SANA NA ALIKUFANYA MAMBO MAKUBWA SANA

WENGINE KILICHOTULETA HAPA ILIKUA MPUNGA NA WASAA WA MPUNGA UKAWADIA HAKIKA WATU WALIKULA NA KUNYWA
WAGENI WAKISUBIRIA MPUNGA KWA HAMU SANA HUKU MEZA ZIKIWA ZIMETAPAKAA VINYWAJI VYA KILA AINA


HATIMAYE WASAA WA MPUNGA NDO HUOOO WATU WALIKULA NA KUSAZA MPKA MPIGA PICHA NIKASAHAU KUPIGA PICHA  DAAAH!!!  USIENDE MBALI SIKUA PEKE YANGU MPIGA PICHA ZIPO PICHA ZA DISCO LA NGUVU LILILOENDELEA HADI MAJOGOO ENDELEA KUFUATILIA VICKY KAMATA BLOG USHUHUDIE USIKU MNENE ULIVYOFANYA KWA DISCO LA NGUVU HUKU WAGENI NA WENYEJI WAKIONYESHANA UJUZI WA KUSAKATA MUZIKI WA KILA AINA.. ................. ENDELEA KUFATILIA VICKY KAMATA BLOG DAIMA.


PAMOJA NA PACHA WAKE ANGELA MSANGI KUTOKA TBC




Monday, 7 July 2014

PICHA: NI NOMA SANA HAYA NDIYO YALIYOTOKEA JANA KATIKA BIRTHDAY PARTY YA MTOTO WA MH. VICKY KAMATA

Na Steven Mruma

         Jana ilikua ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wa Mh. Vicky Kamata na kama kawaida lilianguka booonge la party nyumbani kwa Mh. Vicky Sinza Vatcan.
        Kuacha tukio zima la Birthday party kuna mambo mengi sana yalitokea mengi yalikua ya kufurahisha sana na wakati mwingine hata kushangaza pia, laikin kwa ujumla wake ilikua ni siku tofauti sana kuwahi kutokea nyumbani kw Mh. Vicky Kamata.
    
      MATUKIO YA PEKEE SANA AMBAYO YATAKUJIA MOJA BAADA YA JINGINE ILI UWEZE KUJUA NI NINI HASA KILITOKEA NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. Disco la nguvu ambalo watu walicheza vya kutosha ikiwemo Mh. Vicky Kamata ambaye alionyesha uwezo mkubwa sana katika kucheza muziki hasa wa kizazi kipya na katika tukio hilo nitakuletea video pamoja na picha zikiwa tayari
  2. Tukio jingine lilikua la maandalizi kufanyika kwa ustadi mkubwa na kwa haraka hali iliyopelekea mpaka Mh. Vicky kusahau kuvaa viatu mara kwa mara na kujikuta kupiga picha na wageni akiwa hana viatu.
  3. Marafiki wengi sana walijitokeza na wengi walipiga nae picha ya pamoja kama kumbukumbu.. si mara zote unaweza kupata nafasi ya kupiga picha na Mh. Vicky kamata
  4. kulikua na mashindano ya kucheza ambayo yalishirikisha zaidi watoto na hakika watoto walionyesha uwezo mkubwa sana japo umri wao ulikua mdogo sana.
  5. Kwa mara ya kwanza Mh. Vicky kamata ali perform wimbo wake mpya wa Moyo wa mtu kichaka na baada ya shoo hiyo alitamka maneno mazito ambayo ningependa uyafaham..  
  6. Muonekano mpya wa nyumba ya Mh. Vicky Kamata na mambo mengi ya kifamilia na jinsi anavyoishi na familia yake, 
   Hayo yalikua ni baadhi tu ya yaliyotokea jana na kila tukio litakujia kwa namna yake na kwa uchambuzi wa kina.. enedelea kufuatilia VICKY KAMATA BLOG PAMOJA NAMI Steven Mruma International article writer

HIZI NI BAADHI YA PICHA CHACHE ZA BIRTHDAY PARTY HIYO NA MATUKIO MENGI YATAKUJIA MUDA SI MREFU

MOJA KATI YA KEKI ZA BIRTHDAY YA MTOTO WA MH. VICKY
KEKI ZILIZOANDALIWA KWA AJILI YA SHUGHULI NZIMA YA BIRTHDAY PARTY
 

WATOTO WAKIJICHANA KABLA YA HAFLA YA BIRTHDAY KUANZA

WATOTO WAKIFANYA YAO

 

STEVEN MRUMA [KATIKATI] PAMOJA NA WANAKATI YA CHAKULA NA VINYWAJI WINNIE KUSHOTO NA PETER KULIA

BAADHI YA PICHA NA WAGENI WAKATI WA MAANDALIZI NA HII NI MOJA KATI YA PICHA NYINGI MH. VICKY KAMATA
MH. VICKY AKIWAGAWAIA WATOTO WALIOJUMUIKA KATIKA BIRTHDAY PARTY YA MWANAE

HAPA NI MWAZNO TU WA SHEREHE HIYO NA MATUKIO MENGI YA KEKI MUZIKI NK ENDELEA KUFATILIA BLOG HII.
PICHA YA PAMOJA NA WADOGO ZAKE [ KULIA NI MUANDISHI WA HABARI ZA BLOG HII Steven Mruma 'Trust']


Thursday, 19 June 2014

TUMIA DAKIKA CHACHE KUSIKILIZA WIMBO MPYA WA MH. VICKY KAMATA "MOYO WA MTU KICHAKA"

   NA Steven Mruma.
   Baada ya tukio la kutofungwa ndoa ya Mh. Vicky Kamata mengi yalizungumzwa yapo mengi yaliongelewa tofauti na kila mtu aliandika kutokana na interst yake na kama ulipata bahati ya kumsikiliza kupitia amplifire ya clouds fm wakati akongea na Simon Simalenga aliweka wazi kwa asilimia kubwa ya nini kilitokea.
    Tukiachana na hilo pata nafasi kusikiliza wimbo wake mpya ambao kwa asilimia kubwa unatokana na tukio zima kwa ujumla.
 

Friday, 6 June 2014

BUNGENI DODOMA: PICHA ZA MH. VICKY KAMATA AKIWA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE.. SIKU CHACHE BAADA YA KUTOKA HOSPITALI.

Na Steven Mruma [Dodoma]

        Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata..       Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
Mh. H. Kigwangala akiwa amemkumbatia Mh. Vicky Kamata baada ya kuingia ukumbi wa Bunge mjini Dododma

Mh. Vicky Kamata akiteta jambo na baadhi ya wabunge wenzake ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Mh Vicky Kamata akiwa amekumbatiwa na mbunge mwenzake
   

Sunday, 25 May 2014

AFYA YA MH. VICKY KAMATA YAZIDI KUIMARIKA. NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAMIMINIKA HOSPITALINI KUMJULIA HALI.

Na Steven Mruma.

     Hali ya Kiafya  ya Mh. Vicky Kamata aliyelazwa siku chache zilizopita, baada ya kuugua saa chache kabla ya Ndoa yake inazidi kuimarika huku ndugu jamaa na marafiki wakifika hospitalini kumjulia hali..
     Asubui na mapema nilifika tena hospitali na kukuta baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliofika hospitalini hapo kumjulia hali Mh. Vicky..
     Akiongelea afya yake Mh. aliendela kuwashukuru wote wanao muombea akiamini Mungu amesikia maombi yao na kwasasa hali yake imezidi kuimarika na anaweza kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Baadhi ya ndugu zake [wadogo zake] waliofika kumjulia hali
Mh. Vicky akiwa mwenye furaha baada ya kuwaona baadhi ya ndugu zake waliofika hospitali kumjulia hali
Kwa ufupi hiyo suti nyeusi ikipambwa na shati jeupe na tai ya dhambarau ndio ilikua ivaliwe siku ya harusi ya Mh. Vicky Kamata. [Pembeni kulia ni mdogo wake Mh. Vicky akiwa na gauni la Dhambarau [pupple] ilikuwa ni sare ya harusi

Mh. Ummy Mwalimu akiwa hospitali alipokuja kumuona rafki yake kipenzi Mh. Vicky Kamata
Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na Mh. Vicky alipomtembelea hospitli mapema Leo
Mh. A. Mshama nae alifika hospitali kumjulia hali rafki yake wa karibu Mh. vicky Kamata

Ijapokuwa alikua Hospitali watu mbalimbali walifika na zawadi zao kuonyesha upendo

GEITA DOCUMENTARY

Contributors