NA Steven Mruma.
Baada ya tukio la kutofungwa ndoa ya Mh. Vicky Kamata mengi yalizungumzwa yapo mengi yaliongelewa tofauti na kila mtu aliandika kutokana na interst yake na kama ulipata bahati ya kumsikiliza kupitia amplifire ya clouds fm wakati akongea na Simon Simalenga aliweka wazi kwa asilimia kubwa ya nini kilitokea.
Tukiachana na hilo pata nafasi kusikiliza wimbo wake mpya ambao kwa asilimia kubwa unatokana na tukio zima kwa ujumla.
Thursday, 19 June 2014
Friday, 6 June 2014
BUNGENI DODOMA: PICHA ZA MH. VICKY KAMATA AKIWA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE.. SIKU CHACHE BAADA YA KUTOKA HOSPITALI.
Na Steven Mruma [Dodoma]
Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata.. Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.![]() |
| Mh. H. Kigwangala akiwa amemkumbatia Mh. Vicky Kamata baada ya kuingia ukumbi wa Bunge mjini Dododma |
![]() |
| Mh. Vicky Kamata akiteta jambo na baadhi ya wabunge wenzake ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma |
![]() |
| Mh Vicky Kamata akiwa amekumbatiwa na mbunge mwenzake |
Wednesday, 28 May 2014
Sunday, 25 May 2014
AFYA YA MH. VICKY KAMATA YAZIDI KUIMARIKA. NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAMIMINIKA HOSPITALINI KUMJULIA HALI.
Na Steven Mruma.
Hali ya Kiafya ya Mh. Vicky Kamata aliyelazwa siku chache zilizopita, baada ya kuugua saa chache kabla ya Ndoa yake inazidi kuimarika huku ndugu jamaa na marafiki wakifika hospitalini kumjulia hali..Asubui na mapema nilifika tena hospitali na kukuta baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliofika hospitalini hapo kumjulia hali Mh. Vicky..
Akiongelea afya yake Mh. aliendela kuwashukuru wote wanao muombea akiamini Mungu amesikia maombi yao na kwasasa hali yake imezidi kuimarika na anaweza kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa.
![]() |
| Baadhi ya ndugu zake [wadogo zake] waliofika kumjulia hali |
![]() |
| Mh. Vicky akiwa mwenye furaha baada ya kuwaona baadhi ya ndugu zake waliofika hospitali kumjulia hali |
![]() |
| Mh. Ummy Mwalimu akiwa hospitali alipokuja kumuona rafki yake kipenzi Mh. Vicky Kamata |
![]() |
| Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na Mh. Vicky alipomtembelea hospitli mapema Leo |
![]() |
| Mh. A. Mshama nae alifika hospitali kumjulia hali rafki yake wa karibu Mh. vicky Kamata |
![]() |
| Ijapokuwa alikua Hospitali watu mbalimbali walifika na zawadi zao kuonyesha upendo |
Saturday, 24 May 2014
PICHA: MH. VICKY KAMATA AKIWA AMELAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA SAA CHACHE KABLA YA NDOA YAKE... HALI YAKE YAZIDI KUIMARIKA PIA SOMA ALICHOKIZUNGUMZA NILIPOMTEMBELEA KUJUA HALI YAKE.
Na Steven Mruma
Ni tukio nadra sana kutokea na mara linapotokea lazima ukubali ukweli na hali halisi, zilibaki saa 36 tu kabla ya kufungwa kwa ndoa ya Mh. Vicky Kamata mbunge wa viti maalum Geita na msanii wa muziki ambaye pia amejizolea umaarufu kwa kutetea haki za wanawake.Ilikua ni jioni ya alhamisi Mh. Vicky alianza kujiskia vibaya na kila muda uliposonga hali yake ilizidi kuwa tete na hatimaye alikimbizwa katika hospitali ya General Hospital iliyopo Tabata Segerea..
Kuugua huko kulifanya ndoa yake kuahirishwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa hataweza kufunga ndoa na sababu kubwa ikiwa ni hali ya maumivu makali ya tumbo, Presha kuwa chini sana na Kutapika sana, Hayo yanatokana na ujauzito alio kuwa nao ambapo isingekua rahisi kwake kuhumili suala zima la ndoa na sherehe yake kwa ujumla kwakua ingehatarisha maisha ya mtoto aliye tumboni, kwani ujauzito huo ungeweza kuharibika na kutoka.
Daktari aliongeza pia presha yake ilikuwa chini sana na alikuwa anatapika sana jambo lililomfanya Mh. Vicky kuishiwa nguvu.
Leo asubuhi nilifika hospitali kwa mara nyingine kujua hali yake na aliweza kuongea na mimi machache na kunieleza kua hali yake imeanza kuimarika na maumivu pia yameanza kupungua na aliweza kuongea vizuri tofauti na hali ya jana ambapo alikuwa hawezi kuongea na kila alipojaribu alionekana kushindwa kuongea sababu ya maumivu makali aliyokuwa anayapata.
" Hali yangu ni nzuri kwakweli namshukuru sana Mungu najiskia vizuri asanteni kwa maombi yenu na natumai hali yangu itaimarika na nitarejea katika hali ya kawaida muda sio mrefu" alisema Mh. Vicky huku akioneka bado anauchovu kidogo.
![]() |
| Na hii ndio Hospitali aliyolazwa Mh. Vicky Kamata |
![]() |
| Mh. Vicky Kmata akiwa amelala hii ilikuwa mara tu nilipoingia wodini alipolazwa na nilisubiri dakika kadhaa na aliweza kuamka na nikazungumza nae. |
![]() |
| Mh. Vicky Kamata akiwa amepunzika wakati nilipofika kumuangalia na kuzungumza nae juu ya hali yake. |
![]() |
| Steven Mruma [mwandishi wa habari hii] kushoto, hapa nikiongea na Mh. Vicky Kamata, ilikua ni baada ya kumuamsha na kujua hali yake ambapo aliamka na tukaanza kuzungumza machache juu ya afya yake. |
![]() |
| Hapa akinielezea hali yake kwa ujumla |
![]() |
| Baada ya Muda baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake nao walifika kutaka kujua hali yake na alionekana mchangamfu sana ikiashiria hali ya afya yake kuimarika . |
![]() |
| Ndugu na Marafiki waliofika kumuona hospitalini leo |
Saturday, 3 May 2014
PICHA ZA MH. VICKY KAMATA NCHINI CHINA KATIKA MAANDALIZI YAKE YA KUANZA MAISHA MAPYA HIVI KARIBUNI. [TUNASUBIRI KWA HAMU]
Na Steven Mruma [Guangzhou China].
![]() |
| MSOSI TIME |
![]() |
| PICHA NDANI YA ASIA INTERNATIONAL HOTEL PAMOJA NA BWANA DALMAR ISMAN WA UK ALPOKUJA CHINA KWA AJILI YA CANTON FAIR NA BWANA MAHDI AMBAYE NI C.E.O. WA ABM GROUP |
![]() |
| WAKIPATA MIXED FRUIT NA BWASHEE NA MARAFIKI |
![]() |
| MH. VICKY, SALAHAA WA SILENT OCEAN NA CHARLES |
![]() |
| NITAKUAMBIA BAADAE KUHUSU HII PICHA |
![]() |
| MH. VICKY , STEVEN [ SIE MUANDISHI WA HABARI HII] NA CHARLES |
![]() |
| MIXED FRUIT JUICE |
![]() |
| NJE YA ASIA INTERNATIONAL HOTEL... |
Subscribe to:
Posts (Atom)

































