Friday, 5 July 2013

OBAMA AFURAHISHWA NA UKARIMU WA WATANZANIA

                               Raisi Barack Obama akipokelewa na umati wa watu
                 
                 Raisi Barack Obama akiwasili katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerer



Wednesday, 3 July 2013

REVO AKIWA NCHINI TURKEY


                                 Revo na rafiki zake wakiwa katika uwanja wa ndege wa istanbul
                                             Huwo ni mti mkubwa kuliko yote nchini Turkey
 Juu hapo ni uwanja wa mpira wa timu maarufu ya uturuki iitwayo galatasary
                     Hapo juu ni moja ya misikiti mkubwaa nchini Turkey uitwao BLUE MOSQUE


Tuesday, 21 May 2013

MSAFARA WA FISTULA INATIBIKA WAELEKEA GEITA



Katika kuelekea kuadhimisha siku ya Fistula Duniani, 23/5/2013, Vodacom kwa kushirikiana na taasisi ys CCBRT wameandaa safari ya kuzunguka nchi nzima inayofahamika kama ‘Fistula Inatibika’ kutokea Bukoba hadi Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya siku hiyo kwenye viwanja vya CCBRT yatakayopokelewa na Rais Jakaya Kikwete.

Safari hiyo ambayo inahusisha pia kupita kwenye sehemu mbalimbali kuwapa wananchi ujumbe kuwa Fistula inatibika, itajumuisha pia kukusanya ujumbe kutoka kwa familia zilizoathirika na Fistula kupeleka kwa Rais hapo tarehe 23 ya mwezi huu.
Msafara huo utakaochukua jumla ya siku saba, unaongozwa na mwanamuziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, ambaye atakuwa akiwapa elimu kuhusiana na Fistula wananchi wa sehemu tofauti tofauti watakaopitiwa na msafara huo.

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Bwana Salim Mwalimu akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwenye kampeni ya Fistula Inatibika

MwanaFA akiwaelimisha wananchi wa Geita na kuwahamasisha kutumia fursa hii kujitokeza ili waweze kutibiwa bure

Familia yenye furaha iliyofanikiwa kuushinda ugonjwa wa Fistula kutokana na juhudi za hospitali ya CCBRT pamoja na Vodacom Foundation

Wakazi wa Geita waliojitokeza kwenye kampeni ya Fistula Inatibika

Habari na bongolookup blog

GEITA DOCUMENTARY

Contributors