Saturday, 7 April 2012

REST IN PEACE STEVEN KANUMBA 'The Great'



Muigizaji maarufu wa filamu za kibongo Steven Kanumba A.K.A Kanumba The Greit amefariki dunia usiku wa manane kuamkia leo, na maiti iko muhimbili. kwa taarifa zilizopo ni kuwa msiba upo Sinza maeneo ya Vatican, ukifika Vatican Hotel umefika msibani. sababu za kifo chake hazijathibitishwa. stay with us kwa habari zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMEN


Jina la kuzaliwaSteven Charles Kanumba
Alizaliwa8 Januari 1984ShinyangaTanzania
Kafariki6 Aprili 2012Dar es SalaamTanzania
Kazi yakeMuigizajiMtunziMtayarishajiMuongozaji

MAISHA
Na ameanza elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja ya jiji Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to LagosShe is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.

Friday, 23 March 2012

Marekebisho ya Anuani ya Victoria Foundation


Victoria Foundation inapenda kuomba radhi kwa makosa ya uchapishaji
Yaliyofanyika katika graphic iliyotumika kwenye blog ya Issa Michuzi
Kutoa shukrani kwa Wafadhili wa Victoria Foundation tarehe 22.03.2012
Katika graphic hiyo inaelekeza kimakosa kuwa ofisi zetu zipo Uhuru Street
Mnazi Mmoja.Taarifa sahihi ni kwamba ofisi zetu zipo Nkrumah Street,
LIDA HOUSE, 2nd Floor.

    "TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOJITOKEZA"

SHUKRANI TOKA VICTORIA FOUNDATION KWA WAFADHILI



MHESHIWA VICKY KAMATA MBUNGE WA GEITA VITI MAALUM NA MWENYEKITI WA VICTORIA FOUNDATION ANAPENDA KUTOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA MAKAMPUNI , TAASISI NA WATU BINAFSI WALIOJITOA KWA HALI NA MALI KUISAIDIA WATOTO YATIMA NA WALEMAVU MKOA WA GEITA, MWENYEZI MUNGU AWARUDISHIE MARA MIA KWA MOYO WAO WA UPENDO.


1.      HOME SHOPPING CENTER
2.      EWURA
3.      QUALITY GROUP LIMITED
4.      TRA
5.      GEITA GOLD MINE
6.      MHESHIMIWA MARK BOMANI
7.      PPF
8.      UDF (UNITY IN DIVERSITY FOUNDATION)
9.      MKURUGENZI HALIMASHAURI YA WILAYA GEITA
10  MERY NOTMAN (KIDSCARE IRELAND)

Wednesday, 14 March 2012

Victoria Foundation Ltd yapata ofisi mpya




Victoria Foundation Ltd imehamisha ofisi yake kutoka Kijitonyama ilipokuwa awali,na sasa zipo 
2nd Floor,LIDA HOUSE, Nkrumah Street.

GEITA DOCUMENTARY

Contributors