Tuesday, 22 March 2011
MAJINA YA WASANII WA 5 STAR WALIOFARIKI KATIKA AJALI
Majina ya mwanamuziki wa kundi la 5 Star waliofariki katika ajali ya gari Mikumi Mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yatajwa.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barbarani mkoani Morogoro Ibrahimu Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti(aliyeimba wimbo wa mchumu chumu mwaa),Nassoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashimu, Tizo, Omary Tall, Ngeleza Hassan, Hamisa Omary, Maimuna, Haji Msaniwa na mcheza show wa kitu Tigo Ilala jijini Dar es Salaam.
Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ni Mwanahawa Ally(55) kutoka kundi la East Africa Melody, Susan Benedict(32), Zena Mohamed(27), Samila Rajabu(22) na Mwanahawa Hamisi(36) wamelazwa wodi namba tatu.
Wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Ally Juma(25), Rajbu Kondo(25), Shabani Hamisi(41), Msafiri Musa(22) na Issa Hamisi.
KUNDI LA TAARABU LA 5 STAR LAPATA AJALI

BAADHI YA WANAMUZIKI WA 5 STAR TAARABU
WANAMUZIKI WA BENDI YA FIVE STAR MODERN TAARABU ZAID YA 10, WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA GARI HUKO MOROGORO ENEO LA MIKUMI NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA HALI ZAO NI MBAYA. GARI HILO LILIKUWA NA WATU 22, LAKINI WAMENUSURIKA 5, HUKU WATATU WAKIWA WAMEUMIA KIDOGO. KWA MUJIBU WA VYANZO VYA HABARI INADAIWA GARI HILO LILIKUWA KWENYE MWENDO MKALI NA KUPELEKEA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEPAKIA MBAO PEMBENI YA BARABARA, KUGONGA HUKO ILIPELEKEA VIFO VYA WATU 8, HAPO HAPO NA KISH AKAENDA UPANDE WA PILI AMBAPO LORI LINGINE LILIKUWA LINATEMBEA NDIPO ILIPOISHIA NA KUSABABISHA VIFO HIVYO ZAIDI YA 10, NA MAJERUHI WENGI.MAITI ZIMEHAARIBIKA VIBAYA SANA HALI AMBAYO HAZITAMBULIKI KUTOKANA KUWA VIWILI WILI. habari kwa hisani ya Andrew Chale(Tanzania Daima)
ANNA MAKINDA ATEMBELEA LIBERIA
Wanawake waishio Liberia wakiwa katika picha ya pamoja na Spika Anna Makinda
Watanzania waishio Liberia wakiwa katika picha ya pamoja na spika Anna Makinda walipomkaribisha chakula cha jioni.
Friday, 11 February 2011
Egypt ya leo
Hosni Mubarak ameamua kung'ang'ania tawi, ameongea kama vile yuko Mtwara. Hosni Mubarak anaonekana kutoelewa kinachoendelea Tahrir na kwingineko Egypt. WaMisri sasa wanaonekana kuwa hawana jinsi. Wataingia mitaani kukata mti. Kama ilivyo kawaida, ukubwa wa moto utakaowaka utaanza kupimwa baada ya swala ya Ijumaa hii leo.(Nam Mdau Maggid Mjengwa)
Subscribe to:
Posts (Atom)

