Uongozi wa juu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
Handeni Mkoani Tanga umekihama Chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Wilaya na Katibu wake pamoja na wanachama 380 ambao wamejiunga na Chama
Cha Mapinduzi (CCM)..
Viongozi hao wa Chadema ni pamoja na Mwenyekiti wa wilaya ya handeni, Luka Selemani, mwenyekiti wa kitongoji cha maguruwe, mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (Chadema) na Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya wilaya.
Wengine ni Katibu wa wilaya hiyo, Athumani Ngido ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu Taifa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Mkoa wa Tanga., Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya wilaya hiyo, Jack son Fransis ambaye pia ni mwenyekiti wa kata ya Kabuku na mgombea udiwani wa Kata hiyo...
Mbali na hao, wamo Mwenyekiti wa Tawi la umoja wa Vijana wa Tawi la Kwamatuku, Abrahaman Mtengwa na mjumbe wa kushughulikia migomo ya chama hicho, Juma Mkomba..
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Bulembo alisema kukimbia kwa viongozi na wanachama hao ni ishara kuu ya chama hicho kusambaratika vipande vipande katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu...
Alisema kadiri siku zinavyokwenda Chadema kitazidi kusambaratika kutokana na baadhi ya viongozi wake kukumbatia madaraka huku wengine wakiachwa wapiga debe.
No comments:
Post a Comment